Nakukosa

wiki mbili zimepita, bila neno wala mnongono,
sijanena na wangu laazizi, wa karibu nayemuenzi,
sautiye kinanda changu, maneno yake nguvu yangu,
Kesha kata tamaa huyu binti?

ulaya kama jokovu, japo nishazoea,
lakini mbona kimya, naogopa mshindo,
lilo mbele silijui, wiki tano zimesalia,
lakini, kesha boeka huyu binti?

la kuamba nalikosa, ewe wangu tausi,
yako sauti i wapi, kinanda kilo tiba,
maskini ua langu, lanawiri lishanyauka?
lakini, huyu binti yuko wapi?

tamati nafika, kitandani naelekea,
nakuwaza na kuwazua, je nirejee kwetu?
heri njema na ikufike, gubigubi ikufunike,
ewe binti uliyenitia kitanzi.

Advertisements

Its a pleasure reading your leave-in

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s