Si Kupanda

Ndugu yangu tahadhari, nakwambia waziwazi,
Usijawe na kiburi, ukachukua vya wizi,
Ukijihisi subiri, utafute lahazizi,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Usijitie mwapuza, kaimba kazi ni kazi,
Tamaa zako punguza, kwanza upate ujuzi,
Ng’ang’ana takuumiza, roho kipenda maizi,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Mapenzi ni njia mbili, upende nawe upendwe,
Mapenzi ya mbwa kali, yasiyopenda yashindwe,
Mapenzi ni ya kibali, asiyependa alindwe,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Kung’ang’ania kukutu, kijuwa
hautapendwa,
Kupigana kwa mtutu, kigundua
umeshindwa,
Kukosa roho ya utu, kwa lazima
unapindwa,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Kioa asokupenda, si kuoa ni kuzoa,
Kifwata alekuwinda, sidhani amekuoa,
Kidhani atakupenda, ni Mungu takuokoa,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Kichapo sio ungwana, hufurahi
uchunguni,
Utajiri siyo zana, ukatumia kuwini,
Usuhuba si laana, ukatesa maskini,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Rafiki ni wa kulinda, mawi yasije karibu,
Adui ni wa kushinda, kanunua kwa taabu,
Ukaishi kumponda, kwani huna
mahabubu,
Kupanda usipopenda, si kupanda ni kutupa.

Like ·  · Share
Advertisements

Its a pleasure reading your leave-in

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s