Acha Nikae Kwenye Mpini

Achana nami,
Nilale kwenye lami,
Huoni napiga lami…
Toka kwangu,
Sitamani wengu,
Naotea mawingu..

Sikaribie nyumbani,
Hukualikwa karamuni,
Ukaja nao wahuni.

Nenda kwako,
Kula vya kwako,
Uyakaliye kitako.

Jichaguliye mji
Wakamia yangu maji ,
Sijisitirie wangu uji .

Tafuta yako kopo,
Sijifanye hapa popo,
Kunyenyekea upepo.

Eti wapiga mwayo,
Kusudi kimoyomoyo,
Utufuate nyayo.

Acha nilale kwenye mpini,
Sinione mimi hayawani,
Hafi njaa niamini.

Advertisements

Its a pleasure reading your leave-in

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s