Rafiki Mnafiki

Sijui ulipo wangu rafiki,
Mbona hivi um’kuwa mnafiki,
Si jana nilipiga mswaki,
Nawe ukawa mhakiki,
Kwamba nil’ofanya ni haki

Kumbe pwagu kapata pwaguzi,
Hila zako sasa zipo wazi,
Kuyatambua tena si kazi,
Matamshiyo sio ya mzazi,
Kunitafuna wanipuliza kiwizi

Yako kaka yanipa wasiwasi,
Ingawaje wewe ni mwenye ukwasi,
Rangiyo mwenzangu nyeusi,
Kama mvua ya kusi
Ridhika nisijekutusi.

Kuvua samaki ukakubali mwenyewe,
Sote tukaandamana au si wewe,
Tukabahatika ukageuka mwewe,
Kwangu ukaanza kurusha mawe,
naapa kutokuamini kamwe,

Haya yetu yanaisha naamini,
Ila mbona fununu yanifikia kwani,
Ulomtendea mwenda zake Athumani,
Wanilimbikizia lawama ya nini,
Ingawaje ukweli unao akilini.

Advertisements

Its a pleasure reading your leave-in

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s